WANANCHI ZANZIBAR WATAKIWA KUSIMAMIA HAKI NA UWADILIFU

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amewataka wananchi kuendelea kumuunga mkono Rais Dk.Hussein Mwinyi katika kusimamia haki za watu wanyonge kwa kusimamia uwadilifu. Mhe. Hemed alieleza hayo wakati akiwasalimia waumini na wakaazi wa Chuini mara baada ya kutekeleza ibada ya sala ya Ijumaa katika Masjid Fatiima chuwini Wilaya ya Magharibi”A”Unguja